IDARA YA WATOTO

Idara hii ilianzishwa kanisani kwa makusudi ya kusaidia malezi ya watoto na pia kusaidia kanisa kujua mahitaji ya msingi ya watoto kwa swala zima la ibada kanisani.

 

Idara inakusudia kuanzisha huduma nyingi zitakazo wavuta watoto kwa Yesu na kuwafanya kuwa wanafunzi wake katika kazi zao za kila siku.

 

Idara hii inakuza imani ya watoto wadogo kuanzia umri wa kuzaliwa mpaka anapofikia umri wa miaka kumi na nne au na tano ili hatimaye aweze kujiunga na kanisa la Mungu.

 

Idara hii inafanya kazi kwa karibu sana na idara ya shule ya sabato kitengo cha watoto na pia idara nyingine kama vile Vijana, kaya na familia, wanawake, na vyama mbalimbali kama Watafuta Njia, Wavumbuzi, n.k.

 

Idara inapaswa kufanya kazi kama kitengo cha wainjilisti kwa kuwatumia watoto kufikisha ujumbe kwa watoto wenzao na hatimaye kwa wazazi ambao sio waumini wetu kwa kupewa mafunzo mbalimbali wakati wa likizo.

 

 Kiongozi wa idara hii anapaswa kuhakikisha watoto wanapewa haki zao za kiibada badala kuwaacha wakiwa wamezagaa huko njewakati ibada ikiendelea kwa watu wazima. Kiongozi anapaswa kwa kushirikiana na mashemasi kuona utulivu wa ibada kanisani.

 

Kiongozi awasiliane na mchungaji au mzee wa kanisa kuona ibada ya watoto inafanyika kila siku kwa kupewa wahudumu; kwa makanisa yasiyo na jengo basi muhubiri akumbushwe kona ya watoto.

Kila kanisa ambalo halina jengo yawapasa kupanga wahubiri wawili kila juma. Wa kwanza ataanza na watoto kwa dakika 7 au kisha muhubiri mwingine atamalizia muda uliosalia. Kama kiongozi weka mikakati kwa kushirikiana na mkuu wa majengo kupata jengo la kuabudia watoto – kwa uendeshaji wa shule ya sabato ya watoto na ibada yao kuu.

Kama kiongozi washirikishe watoto kwa kushirikiana na wazee wa kanisa kuona vipawa vya watoto mapema na kuwapa majukumu ya kanisa mapema ili waanze kulipenda kanisa tangu utotoni. Mfano kuendesha shule ya sabato, kuhubiri siku zao maalumu, programu za mchana za watoto, n.k

 Kuandaliwa efoti za wiki moja au siku nane ambazo zitaendeshwa na watoto. Mahuburi yao maalumu na miongozo ya kufundisha vipindi vya afya. Imegundulika program hizi zimeleta wengi kanisani wakubwa kwa wadogo katika maeneo zilipofanyika.